October 2, 2019


SCOLASTIKA Ngwalueson ambaye mkazi wa Mbagala jiji la Dar es Salaam leo alikabidhiwa Sh Mil. 260 za Jackpot Bonus ya SportPesa.

Ngwalueson alikabidhiwa fedha hizo kwenye hafla fupi iliyofanyika kwake Mbagala Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Mshindi huyo mwenye umri wa miaka amejishindia kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi hicho, Ngwalueson alisema kuwa alianza kubashiri na SportPesa takribani mwezi na nusu uliopita na alipata hamasa zaidi baada ya kuona washindi wa jackpot wa kitita cha Sh Mil. 825.

“Nilianza mchezo huu wa kubashiri mwezi na nusu uliopita na kwa wiki iliyopita niliweka mikeka mitatu ya Shilingi 2000 na mkeka mmoja ukafanikiwa. Hata hivyo, kulingana na kutokujua vizuri mpira wa miguu, huwa nabashiri kwa msaada wa kakangu ambaye ni mpenzi sana wa mpira na kwa leo nimeambatana naye hapa.

“Mimi huwa naweka pesa lakini kaka yangu hunisaidia kubashiri, naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa kwani imeweza kubadilisha maisha yangu. Kwa kila siku nilikuwa nafanya biashara ya kuuza mihogo ili kuendesha maisha lakini nitafanya biashara ambayo angalau itakuwa na uwezo wa kunilipa vizuri, alisema.

“Leo ndio nimeamini kuwa mimi ni mshindi wa jackpot kwa wiki hii licha ya SportPesa kunipa taarifa Jumapili jioni.

“Naomba nichukue fursa hii kuwaatarifu Watanzania kuwa ni ukweli kabisa SportPesa inatoa zawadi kila mshindi anapopatikana na hivyo niwaombe Watanzania na hasa wale ambao bado hawajaanza kucheza na SportPesa wafanye hivyo kwani wanaweza kupata bahati kama mimi ya kujishindia jackpot kama hii.

Kwa upande wake, Edger ambaye ni kaka wa mshindi huyo na ambaye alikuwa akimsaidia kubashiri kwa muda wote huo, alisema  kwa muda wote alikuwa na imani kuwa kuna siku ambapo ndugu yake  ataibuka kuwa mshindi. “Naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru SportPesa kwa kutuwezesha kushinda mamilioni haya ambayo nina uhakika yatabadilisha maisha yetu, aliongeza.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi mfano huo wa hundi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas aliwapongeza kwa ushindi huo na akawashukuru kwa kubashiri na kucheza kwa kupitia SportPesa.

“Tumefarijika sana kuona tumepata mshindi kutoka kwenye familia ya hali ya kawaida na hii ni ishara ya kukwamuka kiuchumi kwa familia nzima.”

“SportPesa tunatoa zawadi kwa kila mshindi wetu ambaye ameshinda bila kuangalia mazingira anayotokea ilimradi awe na umri kuanzia miaka kumi na nane (18).

“Napenda kuwashukuru washindi wetu wa wiki hii na kuwaomba watume vyema pesa walizojishindia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.”

“Tunajivunia sana kwa kuendelea kutengeneza mamilionea wapya kila siku kwani sio Jackpot tu hata huduma zetu zingine ambapo mbali na washindi wa Jackpot wiki hii tumetoa bonasi ya washindi waliobashiri kwa usahihi mechi kuanzia 10 hadi 12.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic