MAURICIO Pochentino, amekiri kuwa wachezaji wake wa Tottenham Hotspur walishindwa kuhimili mikikimikiki ya wapinzani wao Bayern Munich na kukubali kichapo kibaya cha mabao 7-2.
Mchezo huo wa UEFA ulianza kwa kasi na amesema walitengeneza nafasi nyingi walishindwa kuzitumia mapema tofauti na wapinzani wao .
Seger Gnabry, winga wa zamani wa Arsenal alikuwa mwiba mkali Kwa Spurs baada ya kutupia jumla ya mabao manne peke yake na kuongeza ugumu kwa wapinzani.
Baada ya Mpira kuisha alikaa na wachezaji ndani ya chumba cha kubadilishia nguo na kuwaeleza hali halisi kwamba wakubaliane na matokeo kutokana na kuboronga.
"Muda tumefungwa walipoteza matumaini na walifikiri ni mwisho wa mchezo, nadhani hatukufanya vizuri kwani ndani ya dakika 82 matokeo ilikuwa ni 4-3.
"Tulikuwa tunapambana kutafuta nafasi ya kupata matokeo chanya ila tulipoteana mwishoni, niliwaambia wiki iliyopita kuwa msimu huu utakuwa mgumu na mambo yameanza mapema," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment