Michuano hii ya CECAFA inafanyika nchini Uganda inaendelea leo na Tanzania ilitinga hatua ya nusu fainali kwa kuinyoosha Uganda jumla ya mabao 4-2.
Katwila amesema kuwa ana imani na vijana watapata matokeo chanya hivyo mashabiki wazidi kuwaombea.
"Maandalizi yetu yapo sawa na imani ni kubwa kwa vijana kufanya vizuri tunaomba mashabiki waendelee kutuombea kwani malengo yetu ni kupata ushindi kwenye kila mchezo," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment