ABDALAH Panzi ‘Dulla Mbabe’ Bingwa wa ubingwa wa Shirikisho la Ngumi za kulipwa
Duniani (WBO) Asia Pacific uzito wa kati (Super Middle) ambao aliupata hivi
karibuni kwa kumtwanga Zulipikaer Maimaitiali raia wa China amesema kuwa kwa
sasa atamchapa kila anayekuja mbele yake.
Ushindi huo ambao umempa heshima Mbabe ulimpa fursa ya
kupeleka mkanda huo bungeni aliupata kwa kumnyoosha mpinnzani wake kwa TK
raundi ya tatu umeipandisha chati Tanzania kwa upande wa ngumi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mbabe amesema kuwa ana
imani na kile ambacho anakifanya kutokana na maandalizi ambayo anayafanya jambo
linalompa matumaini kuwafundisha adabu mabondia watakaohitaji kupambana naye.
“Mchina amenijenga na kunipa uwezo mkubwa wa kujiamini na kuona
kwamba nami pia nina uwezo wa kupeperusha bendera ya Taifa kimataifa, kazi
yangu kwa sasa kila atakayejichanganya kwenye anga zangu ni lazima nitamyoosha
bila kuogopa,” amesema Mbabe.
0 COMMENTS:
Post a Comment