October 13, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wapinzani wao Pyramids kutoka Misri wajiandae kuchapwa mabao matatu uwanja wa CCM Kirumba kabla ya marudiano.

Yanga itamenyana na Pyramids Octoba 27 kwenye mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kombe la Shirikisho kabla ya kurudiana nao nchini Misri.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejipanga kuifunga Pyramids mabao matatu ya haraka kabla ya kuwafuata kwao.

"Tunahitaji kuwafunga mabao matatu fasta kabla ya kuwafuata kwao, tuna kazi kubwa ya kufanya ila inawezekana na hatutawaangusha mashabiki.

"Tunahitaji kupunguza kazi ya kuwafuata tukiwa na mzigo mkubwa ugenini tukianza kuwafunga mabao mengi haa itakuwa rahisi kushinda kwao, huko tutawaiga moja kisha tunaweka ukuta mzito," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic