HASSAN Mwakinyo, bondia namba moja kwa Afrika kwenye uzito
wa Super Welterweight kg 69 na namba 19 duniani amesema kuwa hana mashaka na
mabondia kutoka Uingereza wala Marekani ambao wamekubali kupanda ulingoni
kwenye pambano la World Class Fight Tanzania.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika Octoba 26 uwanja wa
Taifa na litarushwa mubashara kwenye baadhi ya vituo vya Televisheni vya Bongo
na vile vya nje kutokana na heshima ya Mwakinyo.
Akizungumza na Kijiwe cha Ndondi, Mwakinyo alisema kuwa
anatambua kwamba Waingereza na mabondia kutoka Marekani wamepania kupambana
naye jambo linalomfanya ajifue zaidi.
“Wanajua aina ya bondia wanayekwenda kupambana naye ana
uwezo wa aina gani hivyo nao wanajipanga kuonyesha uwezo wao nitawaumbua mapema
kabisa kwani nitakuwa nyumbani na mashabiki wangu, hili litakuwa pambano langu
la kwanza nyumbani ni lazima nifanye mambo makubwa.
“Kuhusu kutaja majina yao kwa sasa naliacha suala hilo kwa
mashabiki, kikubwa sapoti ni muhimu kwa mashabiki,” amesema Mwakinyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment