UONGOZI wa
timu ya Polisi Tanzania umesema kuwa wachezaji wake wote leo wataogelea minoti
na zawadi za kutosha endapo wataifunga timu ya Yanga ambayo mlinda mlango wao
namba moja na Metacha Mnata.
Polisi
Tanzania inacheza leo na Yanga uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wao wa tatu
msimu huu, imeshinda mmoja mbele ya Coastal Union na kupoteza mchezo mmoja
mbele ya Ruvu Shooting.
Habari
zinaeleza kuwa wachezaji wote wamewekewa mezani dau lisilopungua la kutosha mezani
kwa ajili ya kuwapa motisha kuwamaliza wapinzani wao leo.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa
wamejipanga kuona wachezaji wanachekelea ushindi wao mbele ya Yanga.
“Tunajua tunacheza
na timu ngumu na kubwa jambo lililotufanya tuwaandae wachezai wetu kisaikolojia
na wanatambua kwamba kuna zawadi zao ambazo tutawapa wakishinda, “
amesema Lukwaro.
Yaani Polisi wanaahidi zawadi kwasababu wanacheza na Yanga, kwanini hawakuahidi kutoa zawadi wakicheza na Ruvu Shooting au Mbeya City???? Yaani hizi ni sababu kwanini mpira wetu haukui kwani Viongozi wanaopewa dhamana hiyo wana mawazo potofu na wanawalemaza wachezaji kwa ahadi za pesa kwaajili ya mechi 1 katika 38 za ligi mwishowe timu inashuka daraja kwani walikamia mechi 2 za Yanga na Simba tu msimu mzima
ReplyDeletekama yanga akizubaa apigwe tu, maana kila timu inatafuta matokeo
ReplyDeleteNasikia kila mmoja kaahidiwa boda boda,duh
ReplyDeletepesa zinatoka simba hivyo hutoona wakiahidiwa pesa pale wanapocheza na simba
ReplyDeletesababu yanga hawana pesa