SAID Ndemla ni mchezaji nyota ndani ya klabu ya Simba ambaye jina lake kwa sasa si miongoni mwa yale yanayotamkwa sana kutokana na kutokuwa na nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Simba.
Mwanzoni Ndemla alikuwa anapata nafasi kikosi cha kwanza ila haikuwa wakati wa Kocha Mkuu Patrick Aussems hii inatokana na mifumo ambayo anaitumia kocha huyo pamoja na mbinu zake.
Achana na mbinu za kocha huyu, bado kuna kitu ambacho kipo kwenye miguu ya Ndemla kama hatashtuka wakati utamuacha na mguu wake utamkataa.
Ukimtazama kwa haraka, Ndemla ni mchezaji ambaye amekata tamaa kutokana na kutojipa nafasi ndani ya Simba kwani mwenyewe aliwahi kukiri kuwa ni ngumu kwake kupata namba ndani ya Simba.
Kwa nini aliamua kusema hivyo, alitazama aina ya wachezaji waliopo ndani ya Simba na akasahau kwamba hao wote waliokuja kwa sasa ndani ya Simba wamemkuta akiwa ni nyota.
Achana na suala la kumkuta ndani ya Simba nazungumzia kipaji halisi ambacho kinaishi kwa muda kwenye miguu ya Ndemla.
Hana papara akiwa ndani ya uwanja kila anachokifanya licha ya kuwa ni kiungo anafikiria kuipa ushindi timu yake.
Mtazame kwenye mechi ambazo amepata nafasi ya kucheza katika mipira mitatu atakayopiga mmoja ni lazima ulenge kwenye lango na anakuwa na hatari wakati hakuna anayemfikiria.
Akiwa nje ya 18 ndipo mguu wake na uwezo wake wa mguu wa kulia unaonekana lakini bado hajazinduka anakubali kuacha uwezo wake kwenye mguu unayeyuka taratibu.
Mkumbuke yule Ndemla aliyecheza na KMC msimu uliopita, mtazame namna alivyomalizia pasi ya Mzamiru Yassin alikuwa nje ya 18 na kwa utulivu kabisa alifanya kweli.
Ndemla kwa sasa unakwama wapi? Ni nani aliyekushikia mguu wako, ni wakati wa kuzinduka na kutafuta namna ya kuufufua uwezo wako mguuni mwako.
Lile tabasamu lako linalotokana na mashuti yako ya mbali inabidi ulirudishe, rudisha hali ya kujiamini na ufanye vizuri zaidi ya jana.
Bado sijapata muda wa kufikiria kuhusu kukaa kwako benchi ndani ya Simba ila nafikiria uwezo wako unavyoyeyuka kwenye mguu wako.
Ndemla amekaa simba kwa shinikizo la mo. Huku kocha hana mpango naye. Upande wa pili walimtaka yeye hakutaka kuondoka. Ngoja aendelee kuupoteza uwezo wake.
ReplyDeleteNdemla ana nafasi pale smba na kitakachombeba ni nizam na ustahamilivu wa hali ya juu. Siku za Ndemla kufanya yake zimefika na sio Ndemla tu, bali Simba ina vijana wengi wazawa ambao nnaimani kukaa kwao kwa muda mrefu na wachezaji wa kigeni wenye uwezo ndani ya benchi bora la ufundi kumewasaidia sana kujifunza mengi kilichobakia ni wao wenyewe kumthibitishia kocha wao lakini kwa uwezo hawa vijana hawa wote wapo bomba.Unamuona Ibrahm Ajibu wa sasa? Mpambanaji, Ananguvu.Hana presha yaani katimia.kwa usumbufu wa Ajibu kwa sasa kwa mabeki ukimueka mbele ya goli basi kama si goli penalt.Unamuona Miraji Athumani? Hata Rashid Juma.Mzamiru. Makuzi ya mwanamichezo wakati mwengine huchukua muda kuimarika na ni busara wakawa wanapewa moyo wa kutokata tamaa badala ya lawama tu.
ReplyDeleteMungu yupamoja nasi simba na wataxheza tuu Kwan mvumilivu hula mbivuu skuzotee
ReplyDelete