WAMBURA WA TFF AIBUKA NA MPYA MAHAKAMANI, AOMBA MSAMAHA
News updates kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni kuhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, kueleza kuwa tayari amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akiomba msamaha na kukiri makosa yake.
Wambura amedai hayo leo Oktoba 2, 2019 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina, kuwa aliandika barua kwa DPP kuomba msamaha na kukiri makosa yake hivyo ameuomba upande wa mashtaka kufuatilia ili aweze kupata haki yake.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amesema suala hilo analifanyia kazi kwa haraka zaidi.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, mwaka huul itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Ikumbukwe kuwa Wambura alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Februari 11, mwaka huu, akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh. mil. 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
0 COMMENTS:
Post a Comment