STRAIKA YANGA ALIAMSHA ALALAMIKIA KUTOPANGWA KIKOSINI, 'KUNA UPENDELEO'
Imeelezwa kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Juma Balinya amesema hafurahii kuendelea kuwekwa nje ya kikosi cha timu hiyo mara kwa mara.
Taarifa zimeeleza kuwa Balinya ametoa kauli hiyo mara baada ya kupata nafasi ya kucheza jana akiingia kutokea benchi katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri.
Taarifa hiyo imesema Balinya ameamua kufunguka hayo huku akidai kuna upendeleo wa upangaji wa kikosi ndani ya timu hiyo jambo ambalo linapelekea yeye kutopata nafasi.
Tangu atue Yanga, Balinya amekuwa akianzia benchi mara nyingi na si sehemu ya kikosi cha kwanza, kitu ambacho kimepelekea kuibuke kwa kauli hiyo.
Mashabiki wanasemaje
Baadhi ya mashabiki wengi wa Yanga wameonekana kuisapoti kauli hiyo huku wakitupa lawama kwa Kocha Mwinyi Zahera kwa namna anavyopanga kikosi.
Wameeleza kuna upendeleo kweli unaoonekana ambao wengi wanasema wachezaji wa kikongo ndiyo wamekuwa wakipewa nafasi zaidi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Hivi kuna wakongo wangapi ndani ya kikosi cha Yanga?
ReplyDeleteWawili .
ReplyDeleteWacongo wawili tu wamesajiliwa Yanga na ni mmoja tu alicheza.Nilivyoelewa mimi ni kuwa hawa wachezaji wote walisajiliwa kwa mapendekezo ya kocha Zahera sasa inakuwaje anajitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe?
DeleteHapo ndipo unajiuliza kwanini Balinya asioneshe uwezo wake anapopewa nafasi alalamike kwenye media? Je kwanini alipoambiwa apunguze uzito hajalisemea?
DeleteTuendelee na mpira wa kwenye media huku tukitegemea miujiza ya kuzifunga timu zilizowekeza mabilioni na wachezaji wa kiwango cha juu kwa wa kwetu wa kuokoteza. Hamasa ina ukomo wake juu ya weledi.
Ukweli hubaki ukweli na uongo hujitenga. Kocha wa yanga anaupendeleo. Kwa nini aliwaacha sibo na Balinya nje mpaka timu ikaboronga? Kocha hajui hata kufanya sub! Anamtoa fei anamuacha makame aliyebolonga muda wote!. Ama kweli kocha wa kikongo kweli!
ReplyDeleteUyo Barinya Wenu Sondo Mlimfananisha Na Kagere Sasa Mnaumbuka Hakuna Cha Birimana Wara Sibobimana Vyura Wamekwama Kwenye Tope
ReplyDeletemi nahisi labda wachezaji hawajalipwa
ReplyDeleteNakumbuka jinsi Yanga walivyomtambulisha Juma Balinya kwa mbwembwe wakidai wamewapora Simba, kumbe wenzao waliwaingiza chaka. Pia wakaenda kumsajili Maybin Kalengo kule Zambia baada ya kusikia Simba wanamtaka Kalengo. Kumbe hawakujua kuwa wenzao walikuwa wanamtaka Kalengo wa Zesco na sio huyu waliyemsajili wao. Ovyooo...
ReplyDeletedhambi ya ubaguzi ni mbaya sana...WAKONGO???
ReplyDeleteKocha kaishiwa mipango, aondoke tu
ReplyDelete