October 28, 2019


Baada ya kichapo cha jana dhidi ya Pyramids Fc ya Misri, inelezwa kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato wa kuachana na Kocha wao Mkuu,Mwinyi Zahera.

Maamuzi hayo yanakuja si baada tu ya mechi ya jana bali pia katika mechi za Ligi Kuu Bara ambapo Yanga imeonekana kutofanya vizuri.

Tetesi zilizopo hivi sasa zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Kocha wa mabingwa hao wa Kihistoria, Mholanzi, Hans van der Pluijm, anaweza akarejea ndani ya timu hiyo muda wowote kuanzia sasa.

Hans aliinoa Yanga kwa mafanikio miaka ya hivi karibuni na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu mara kadhaa ambapo sasa anatajwa kutua tena Jangwani.

Hans mara ya mwisho alikuwa Kocha wa Azam FC ambayo ilimtimua mapema baada ya kuingia naye mkataba kutokana na kufanya vibaya kwenye mechi za ligi.

4 COMMENTS:

  1. Kwahilo hata me nawaunga mkono team inacheza hata haieleweke inatafuta Nini

    ReplyDelete
  2. Ni wakati sahihi kabla ya shari haijatokea mabadiliko ni muda muafaka kwa maslahi mapana ya Yanga.

    ReplyDelete
  3. Mi naona papa atuachie timu yet

    ReplyDelete
  4. Bora babu arudi aturudishie furaha wanayanga maana tumekuwa watu wasio na uhakika wa kesho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic