TAMBWE AZUNGUMZIA MAISHA NJE YA YANGA
Hivi karibuni aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe alijiunga na timu ya Fanja ya nchini Oman na ataitumikia kwa mkataba wa miaka miwili.
Hata hivyo, Tambwe ambaye anashikilia rekodi ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara mara mbili, ameliambia Championi Ijumaa kuwa anafurahia maisha ya nchini humo.
Alisema kuwa tangu ajiunge na timu hiyo, mambo yake yamekuwa yakimwendea vizuri na kujikuta akisahau kabisa changamoto alizokuwa akikumbana nazo wakati alipokuwa Yanga. “Namshukuru Mungu maisha yangu huku ni mazuri na ninaendelea kupambana kuhakikisha nafanya vizuri kama ilivyokuwa Tanzania.
“Sina wasiwasi wowote kwani nalipwa vizuri, hela ambayo nachukua ni kubwa kushinda ile niliyokuwa nikichukua Yanga kwa hiyo kila kitu naona kinaenda vizuri,” alisema Tambwe ambaye tayari ameshaitumikia timu hiyo katika mechi mbili za ligi kuu ya nchi hiyo kati ya nne lakini bado hajafunga bao lolote.
0 COMMENTS:
Post a Comment