USHAURI WA SALEH ALLY KWA YANGA DHIDI YA WAZEE WA FITINA
Hadithi kubwa sasa ni Pyramids ya Misri, hii ni kwa kuwa Ligi Kuu Bara imesimama na mwakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ni Yanga.
Hadithi hii si ya KUTISHA, badala yake ina uhalisia unaofanana kwa kuwa timu za Misri hazijawahi kuwa dhaifu dhidi ya timu zetu na mara moja 2003, Simba waliwang'oa Zamalek wakiwa Mabingwa na timu bora Afrika.
Hivyo kila timu ya Misri iwe Al Ahly, Zamalek na nyingine zimekuwa imara dhidi ya zetu hapa nyumbani na si kwa Yanga pekee.
Yanga hawapaswi kuogopa badala ya kuamini kuwa watakutana na timu ya Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika ambao ni bora zaidi, hivyo haitakuwa mechi nyepesi na wanapaswa kujiandaa haswaa.
Pyramids ni imara kwa kuwa imejengwa kwenye msingi ya ushindani dhidi ya Al Ahly baada ya mmiliki wake wa sasa kujiondoa Ahly akiona amedharauliwa.
Pyramids itacheza na Yanga ikiamini inashindana na Ahly. Hivyo si mechi nyepesi lakini kama maandalizi yatakuwa bora, Yanga watakuwa na nafasi ya kuilainisha hiyo mechi na ili iwe hivyo lazima kuwa na USHINDI BORA NYUMBANI maana Misri miaka yote ni pagumu.
hii timu nzuri sana kiuchezaji lakini haina mashabiki misri
ReplyDelete