YANGA WAIPOTEZEA CAF DROO YA MAKUNDI, MWAKALEBELA AFUNGUKA
Uongozi wa klabu ya Yanga umeshindwa kupeleka mwakilishi katika Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kutokana na hatua ambayo wataanza nayo baada ya droo.
Leo kunafanyika droo ya timu zitakazocheza kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema kuwa Yanga hawajaona kupeleka mwakilishi sababu hatua hiyo haina kipaumbele sana kwao.
Ameeleza kuwa watapeleka pindi watakapopata nafasi ya kucheza makundi maana ni hatua kubwa ambayo inapewa kipaumbele kikubwa.
"Ni kweli hatujapeleka mwakilishi CAF sababu hatua ya sasa haina kipaumbele kikubwa kwetu.
"Kama tukifanikiwa kutinga makundi tutapanga nani aende kwa ajili ya kutuwakilisha lakini si sasa."
hakika ukipata kiongozi wa namna hii bora usiwe na uongozi.
ReplyDeletesasa unatinga vipi makundi kama hujacheza hizi gemu za mtoano?
mi hatari sana,harafu inaonekana waz kiwa hana hata chembe ya uhakika wa kutinga makundi
Kiongoz anaogopa droo
ReplyDeletehawa viongozi wa yanga hawaweki nguvu nje bali ligi tu. Yanga imeshindwa kuelewa Hela ipo CAF na sio Ubinnwa wa ki-historia. Mimi Yanga pia. Lakini viongozi hawa bure tu
ReplyDeleteONGEA MAMBO YA KWELI MWENYEKITI WA YANGA TAYARI YUPO MISRI KUFATILIA UPANGAJI WA MAKUNDI ACHA KUTUBABAISHA TUMIA AKILI KUPOSTI VITU
ReplyDelete