October 9, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utacheza mechi za kirafiki kipindi hiki ligi ikiwa imesimama kwa muda.

Yanga imeanza mazoezi leo kwenye uwanja wa Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi zijazo za ligi sambamba na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela amesema timu itacheza mechi mbili za kirafiki ili kuwafanya wachezaji kuendeleza utimamu wa mwili sababu hakutakuwa na mechi za ligi.

Ameeleza wao wanaendelea kujipanga vema kwasababu wana mzigo mrefu huko mbele haswa katika mashindano ya kimataifa hivyo hawana sababu ya kukaa bila kucheza mechi.

"Hivi leo timu imeanza mazoezi kujiandaa na mechi za CAF sambamba na ligi.

"Lengo ni kuwaweka wachezaji wetu fiti sababu hawawezi kukaa bila kucheza."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic