YANGA YAFIKISHWA KAMATI YA SHERIA KISA MADENI YA WACHEZAJI
Kufuatia waliokuwa wachezaji wa Klabu ya Yanga kufikisha malalamiko yao katika Chama cha Haki za Wachezaji Tanzania (Sputanza), klabu hiyo imejikuta ikifikishwa katika Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kujibu mashitaka
Wachezaji hao ambao ni pamoja na Pato Ngonyani, Mwinyi Haji na Antony Matheo walipeleka malalamiko ya kudai fedha zao za mishahara ya miezi miwili pamoja na ya usajili
Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki amesema wamepokea malalamiko kutoka kwa wachezaji hao ambapo tayari wameshayawasilisha kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa ajili ya kufanyia kazi
Kikapu kimetoboka au???Au watu wameanza kutafuna?Si mlisema umaskini nä kutembeza bakuli basi.Andrew Vincent när anadai.
ReplyDeletekatika ukweli ni kazima muwe wakweli.
ReplyDeletemfumo huo yanga madeni kila siku.
jambo la kushangaza,mbona timu ndogo htusikii malalamiko haya? timu kubwa haina mipango?
kila siku makelele kumbe madeni bado
YANGA walikuwa washtakiwe zamani tu hata FIFA.
ReplyDeleteEti GSM ametowa milioni 10 goli lenyewe mmeliona wenzangu la kupewa kabisa halafu eti wameshinda wanapewa na hao gsm eti m 10 hakuna timu hapo
ReplyDelete