KIKOSI cha
Yanga chenye mabadiliko makubwa msimu huu kimeshindwa kuivunja rekodi yake ya
msimu uliopita ya 2018/19 kwa kuipoteza kabisa rekodi yao ya msimu uliopita.
Rekodi
zinaonyesha kwamba msimu wa 2018/19 Yanga ikiwa na staa mkubwa Heritier Makambo
pekee kwenye mechi nne sawa na dakika 360 walivuna jumla ya point 12 na
walikuwa vinara wa ligi kwani hawakupoteza mchezo hata mmoja.
Yanga
iliyokuwa inaongozwa na Kelvin Yondan akiwa ni nahodha mkuu kabla ya kupigwa
chini ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar mabao 2-1 ikaipiga Stand United mabao 4-3
kabla ya kuikandamiza Coastal Union bao 1-0 na ikashushia pumzi kwa Singida United kwa mabao 2-0.
Kwenye mechi
nne Yanga ilifunga jumla ya mabao 9 na ilikubali kufungwa mabao manne pekee
huku beki wa kwanza kufunga bao kwa msimu huo ndani ya Yanga akiwa ni Kelvin
Yondan aliyefunga dakika ya 40 kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa penalti
na mechi zote zilichezwa uwanja wa Taifa.
Mambo
yamekuwa tofauti msimu huu ambapo Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera
ina mastaa wa kutosha ikiwa ni pamoja na David Molinga mtaalamu wa kupiga
mipira iliyokufa pamoja na beki mwili jumba Lamine Moro imeambulia jumla ya
pointi 7 ikizipoteza pointi 4.
Imefunga
jumla ya mabao sita na imefungwa mabao manne ndani ya dakika 360, mchezo wake
wa kwanza ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting uwanja wa Uhuru kabla ya
kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na Polisi Tanzania na ilishinda mbele
ya Coastal Union bao 1-0 na mbele ya Mbao FC bao 1-0.
Zahera
amesema kuwa mabadiliko makubwa ndani ya kikosi yanaifanya timu yake kushindwa
kupata matokeo kutokana na kukosa muunganiko mzuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment