ARSENAL YAFANYA MAZUNGUMZO NA KOCHA MPYA KUTOKA BARCELONA
Klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuhusu mpango kuchukua nafasi ya Unai Emery. (El Confidencial, kupitia Metro)
Klabu ya Tottenham wapo tayari kutoa ofa ya pauni 50m kwa Memphis Depay mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alihamia Klabu ya Ufaransa Lyon kutoka Manchester United mnamo Januari 2017.(Sunday Mirror)
Manchester United inajipanga kumsajili tena mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, katika msimu ujao wa kiangazi. (The Sun on Sunday)
Chelsea inataka kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 24, kama adhabu ya kufungiwa itafutwa mwezi Januari. (Sunday Mirror)
Pia timu ya Chelsea wanataka $ 5m kutoka kwa klabu yoyote inayotaka kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud, 33, mnamo Januari.(Sunday Express)
Paris St-Germain kwa mara ya kwanza wamefanya majadilano ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappé lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa. (L'Equipe, via Marca)
Meneja wa Liverpool Jürgen Klopp hayupo tayari kumuachia Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 30, aondoke klabuni hapo kwenye dirisha dogo la uhamisho Januari.(Football Insider)
Juventus wanaweza kuwatoa wachezaji wake wanne kwenda Manchester United akiwemo mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic, 33, kiungo wa Ujerumani Emre Can, 25, beki wa Italia, Dani Rugani, 25, na kiungo wa Ufaransa, Blaise Matuidi, 32, kubadilishana na kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Tuttosport, kupitia Sunday Express)
Manchester City ipo tayari kumpatia Mholanzi Giovanni van Bronckhorst fursa ya kufanyiwa majaribio kama mrithi wa Pep Guardiola kwa kumteua kuwa kocha kwa klabu mwenza New York. (Sunday Mirror)
Everton inapokea maombi ya kumuuza kipa wa Uholanzi Maarten Stekelenburg Januari, huku mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu. (Football Insider)
Wolves watakamilisha usajili wa mlinzi mwenye umri wa miaka 17 wa PSV Eindhoven, Nigel Lonwijk kwa kitita cha £200,000 ifikapo Januari. (ED, via Birmingham Mail)
Uefa inatazamia kuandaa fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya 2024 nchini Marekani, huku New York ukiwa ndio mji unaopigiwa upatu katika hatua itakayochangia mechi hiyo kuchezwa kwa mara ya kwanza nje ya Ulaya. (Morning Consult)
0 COMMENTS:
Post a Comment