PANGA KUPITA SIMBA, USAJILI WA NGUVU KUFANYIKA DIRISHA DOGO
Inaelezwa kuwa aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Simba ambaye sasa ni mshauri wa Mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, Crescentius Magori, ameshauri kufanyike usajili wa nguvu dirisha dogo.
Magori amependekeza Simba wafanye usajili dirisha dogo ili kupata wachezaji ambao wataisaidia klabu kuelekea michuano ya kimataifa msimu ujao.
Inaelezwa sababu ya Magori kutoa pendekezo hilo ni kuisaidia Simba kupata wachezaji kwa gharama nafuu tofauti na kipindi cha dirisha kubwa.
Taarifa imeeleza, Magori anaamini usajili huo utaisaidia Simba kunako mashindano ya kimataifa baada ya kushindwa msimu huu kwa kutolewa mapema na UD Songo.
Kwa namna hali inavyoonekana, kuna uwezekano baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi cha Simba wataachwa endapo usajili huo utafanyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment