November 10, 2019


Beki wa zamani kunako timu ya Yanga, Bakari Malima, amesema kuwa alisajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria kwa kiasi cha shilingi laki tano.

Malima amefunguka hayo kupitia kipindi cha Njia Panda ya Clouds FM wakati akihojiwa na Dr. Isack Maro.

Amesema kuwa fedha hiyo ilikuwa ni kubwa kwa kipindi hicho na alisajiliwa wakati akitokea Pan African.

Beki huyo maarufu kwa jina la Jembe Ulaya, anakumbukwa kwa umaridadi na ushajaa wake wakati akisakata gozi.

Malima hivi sasa amekuwa akijihusisha na biashara mbalimbali pamoja na uchambuzi wa soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic