YANGA YATOA DOZI YA MAANA MTWARA, YAITANGWA NANYUMBU 5-0
Kikosi cha yanga kimeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Nyamumbu Combine kutoka Mtwara.
Ushindi huo umepatika katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani humo.
Katika kikosi cha leo, asilimia kubwa ya wachezaji wa yanga walikuwa ni wale wa kikosi cha vijana.
Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Adam Stanley aliyefunga mabao matatu huku Marcelo akifungwa kwa penati bao moja na jingine likifungwa na James Wilson.
0 COMMENTS:
Post a Comment