LIVERPOOL leo imesubiri mpaka dakika ya 49 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Sadio Mane kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.
Wilfried Zaha hakuwa mnyonge aliandika bao la kusawazisha dakika ya 82 Kwa Crystal palece ambalo lilidumu kwa muda wa dakika tatu pekee.
Robert Firmino mshambuliaji wa Liverpool alimaliza kazi ya mwisho dakika ya 85 na kufunga bao la ushindi kwa Liverpool.
Mane anafikisha bao la nane ndani ya Ligi Kuu England huku Firmino akifunga bao lake la nne.
Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe jumla ya pointi 37 ikiwa kileleni huku Crystal Palace ikiwa nafasi ya 13 na ina pointi 15 kwa sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment