KISA MAMILIONI, YANGA WAMSHANGAA DANTE KWENDA TFF, UONGOZI WATOA TAMKO
Uongozi wa klabu ya yanga umeshangazwa na maamuzi ya mchezaji wao Andrew Vincent 'Dante' kufungua mashtaka ya kudai fedha zake ambazo ni zaidi ya milioni 45 katika Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF).
Dante alifikia maamuzi hayo baada ya kuona fedha zake hazilipwi hivyo kuamua kuangalia sehemu nyingine ya kudai haki yake na ndipo aliona TFF panafaa.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ameeleza kuwa kwa namna hali yao ilivyo ndani ya klabu yao ni ngumu kumlipa Dante kiasi chote hicho cha pesa.
Amesema hapo awali walikubaliana naye kuwa watakuwa wanalipana kidogokidogo lakini baadaye wamekuja kushangazwa na namna alivyoamua kwenda TFF kushtaki.
"Ujue sisi na Dante awali tulikubaliana naye tuwe tunamlipa kidogokigo.
"Kwa kiasi cha pesa aliyonayo na hali iliyopo Yanga ni ngumu kumlipa fedha yake yote.
"Tunashangaa kuona amekimbilia TFF ambao hawawezi hata kumpa fedha hiyo labda wawe wanakata kutokana na mapato ya uwanjani."
ReplyDeleteWANAYANGA PATENI MAJIBU AMBAYO NI HAKI YENU KWA HAYA YAFUATAYO
🔛Ningependa kuwashauri wanayanga kuulizia na kufahamu mambo yafuatayo ambayo bado yanautata....ambayo wengi hawajapata majibu yanayoridhisha na yasipopatikana yanaweza "kuchafua hali ya hewa" pale mtaa wa Twiga & Jangwani.
⛔ Kocha Mkuu & Benchi La Ufundi lililo Bora na La Kisasa
Baada ya Kuondolewa na Kuvunjiwa Mkataba Mwalimu Mwinyi Zahera na Msaidizi wake Noeli Mwandila na Benchi lote ka Ufundi...Liliundwa benchi la muda likiongozwa na Charles Boniface Mkwassa akisaidiana na Saidi Maulidi SMG.....hawa waliambiwa wanashikilia timu kwa Wiki 2 wakati ambapo Kocha wa Kudumu anatafutwa.
Ukiangalia Ligi Kuu ilivyo...na Malengo ya Klabu kuchukua ubingwa....lazima apatikane Kocha Mkuu mwenye kiwango zaidi ya Mkwassa kwani kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza Zahera ikiwa hawakuweza kumpata mwalimu mwenye uwezo wa juu zaidi ya Mkwassa....bado ili timu ishindane kwa ubora na uimara katika kiuchezaji na timu kama Simba au Azam lazima Kocha wa Kudumu awe anatokea katika nchi zilizo na uwezo na utaalamu wa kufundisha soka zaidi ya walimu wanatokea ukanda huu wa Afrika (Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi)
⛔ Ushauri Kuhusu Kocha
Kocha wanaotokea Serbia, Yugoslavia, Scotland, Amerika Kusini ama Ulaya Magharibi watafaa kuifundisha Yanga kwani Timu inatakiwa iimarike kiuchezaji na kifalsafa
⛔ Kuacha Visingizio Vya Ukosefu wa Pesa
Kuna dhana inayojengeka kuwa Timu haina fedha kwa hiyo tuiishie kufundishwa na wazawa ambao uwezo wao ni wa kawaida hii ni dhana potofu ambayo haina ukweli wowote. Yanga ni timu kubwa ambayo ina udhamini wa makampuni zaidi ya 4 (SportPesa, Taifa Gas, GSM, Maji ya Afya, Azam Media) pamoja na Vodacom....pili Yanga ina wanachama na mashabiki wenye uwezo mkubwa wa kifedha wanaojitolea kuilipia gharama kubwa kubwa mifano mingi ipo kudhihirisha hili kama ambavyo ilivyofanyika huko nyuma. Isitoshe, Kuendana na Ukubwa wa Jina la Yanga na msukumo unaotokana na Uwekezaji uliofanyika Simba itakuwa ni aibu kwa Yanga kutoingia kwenye mabadiliko ya kiundeshaji na kupata mwekezaji ama wawekezaji/ ambao wana uwezo kuzidi hata huyo aliyepo Simba...
⛔ Uwanja wa Kaunda na Kigamboni
Kumekuwa na kusuasua na mwendo wa kinyonga katika utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa Yanga. Wapenzi na Mashabiki wanahoji hili na hasa wanapoona wenzao mtaa wa Pili wao wamekamilisha uwanja wao...ila Yanga zimebaki porojo na siasa tu....ILI LAZIMA LIISHE WANAYANGA WAMECHOKA WANATAKA VITENDO
🚫 Maswali
✔ Kwanini kuna kusuasua na kujivutavuta kuingia katika Uwekezaji na Mabadiliko katika Yanga huku kukiwa kushindwa Kamati lukuki zilizo leta mabadiliko au kufanya Vitendo vinavyoonekana?
✔ Je, Viongozi wana nia ya dhati ya kuiinua Yanga kiuchumi? Kama wanayo mbona mchakato wa mabadiliko unachelewa?
✔ Je, Kama hauchelewi na kama haurakishwi kwanini kuna kilio cha ukata wa fedha na kutaka "KUENDESHA MAMBO KIZAMANI KWA MFUMO WA KARNE YA 19 WAKATI TUPO KARNE YA 21???? Mpira ni Pesa na Matokeo mazuri na uendeshaji wa Timu kwamaana ya Benchi la Bora la Ufundi, Miundo Mbinu Bora, Kambi na Huduma za Wachezaji Bora hutokana na Uwekezaji wa Pesa....kwani Uongozi uliochaguliwa ulisema ndani ya Miezi 3 hadi 6 wataiingiza Yanga katika mabadiliko hili mbona unasuasua???
🚫 Wenu katika kutoa ushauri chanya kwa ajili ya Maendeleo ya Mpira Tanzania!
Ahsanteni
Vipi Hali ngumu kwani so mnayo mamilioni ya GSMo ma huku
ReplyDeletemunatangaza kuwajaza mamilioni wachezaji kila wanaposhinda mechi na kuchota wachezaji na makocha wa mamilioni na kuwafukuza na kuleta wengine wa bei kuliko hizo na leo hii eti kumshangaa huyo kijana anapodai mamilioni Yake.Mlipe kibaruwa ajira Yake kabla ya kukauka jasho lake na mkate makoti Kwa mujibu wa kitambaa ulichkuwanachov
Kijana elewa pesa za mdhamini sio kulipa madeni,wanaotakiwa kumlipa Dante ni viongozi wa timu na wao wameshatamka watalipa kiduchu kiduchu kwani hali yao sio mujarabu.Bahashishi anayotoa GSM kwa kila mechi haipo kwenye makubaliano na Yanga kwani anaweza sitisha wakati wowote.
DeleteJamani vyura vyura vyura Mungu anawaona hizo za kumlipa zahera faster faster zilitoka wapi. Sii haki na inauma sana.Mnasema timu haifanikiwi kwa uzurumati wa namna hii duuuù hamna kitu,chozi la kijana huyu ni laana kwenu make mlijua.
ReplyDeleteMsitaraji baraka Kwa kudhulumu dhulma itazidi mikosi na kukipelekeni pabaya na ikiwa kumlipa kiduchukiduchu ilihitaji makubaliano tokea mwanzo Dio kushitukis Tu na huku kijana akishuhudia akina Molinga na Balanya na wengineo wakikabidhiwa mamilioni na wengine kati ya hao wakitimuliwa na vyao kupewa na kuahidi badala kuletwa na kijana akiyashuhudia hayo Kwa Kweli i inauma.
ReplyDeleteHivi inakuwaje mnalipa Mamilioni ya pasa kwa usajili mpya hasa kwa Wachezaji wa Kigeni, huku Dante aliyeitumikia Club kwa jasho na damu, mshindwe kumlipa??? Yanga. Mlipeni kijana wa Watu fedha zake. Acheni dhuluma.
ReplyDeleteuhongozi huu nao jipu tu tusubili muda wake kitanuka tu
ReplyDeleteKama bata mzinga kujitunisha akawa kama tembo kumbe ni manyoya Tu Hanna chochote. Ikiwa Dante na Zahera mnashindwa kuwalipa vipi mtaweza kumlipa mnaemtaka ambae Bosi wa Zahera na ikiwa mnao uwezo wa kumlipa kwanini hamumlipi Dante au inangojewa anyamaze na asahau mojakwamoja. Ubingwa munaouotaka ndio mtaupata Kwa kudhulumu wengine?
ReplyDeleteYanga wanakabiliwa na mechi 2 za viporo lakini kwa mshangao wa wengi Viongozi wamewaruhusu kwenda kuingia kambini kwenye timu ya Taifa Zanzibar. Hili ni kosa kwani safu ya kiungo ya Timu ya Yanga itakuwa na mapungufu....hii ni Kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi kama vile Mapinduzi Balama. Nawasihi Viongozi Tafadhali warudisheni wachezaji wa viungo walioenda Zanzibar......
ReplyDeleteAhsanteni
Si kila mkishinda mechi gsm anawapa milioni 10 na mkitufunga ss mnyama nimesikia mtapewa milioni 100 kandambili ya chooni hiyo mnaloooooo hilo mlipeni hiyo dante
ReplyDelete