November 23, 2019


Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga, leo Jumamosi itakutana kwa ajili ya kumjadili mrithi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

Zahera alivunjiwa mkataba wake na Yanga kutokana na matokeo mabovu ambayo kikosi hicho ilikuwa ikiyapata na sasa timu ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

Taarifa ambazo Championi Jumamosi lilizipata zinadai kuwa, kamati hivyo itazipitia CV zote ambazo zinatajwa kufikia 40 ambazo wamezipokea hivi karibuni ikiwemo ya Kocha Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu.

Shungu aliliambia Championi kuwa: “Tayari nilishawatumia CV yangu viongozi wa Yanga, hapo awali tuliongea na niliwatajia mshahara ambao nauhitaji lakini hatukukubaliana kuhusu hilo, kama watakuwa tayari nadhani tutaendelea kuwasiliana, imebaki upande wao maana kwa upande wangu tayari nishamaliza ambapo ni kutuma CV.”

Shungu ambaye aliwahi kuinoa Yanga mwaka 1998 hadi 2001 na kuipa ubingwa wa ligi, aliwatajia viongozi wa timu hiyo mshahara wa Sh mil 25 kwa mwezi kitu ambacho kiliwafanya watikise kichwa wakijifikiria zaidi kwani Zahera alikuwa akipata Sh mil 7 kwa mwezi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alithibitisha uwepo wa kikao hicho: “Kuna kikao cha kamati ya utendaji ambacho kitakaa Jumamosi (leo) kujadi.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic