November 23, 2019


HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa mshambuliaji wao kipenzi Mnyarwanda, Meddie Kagere amerejea nchini na fasta akaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Hiyo ni baada ya mshambuliaji huyo kukosekana kwenye mazoezi ya juzi Alhamisi asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Ruvu utakaopigwa leo kwenye uwanja huo.

Awali, ilielezwa kuwa huenda mshambuliaji huyo tegemeo wa Simba mwenye mabao nane asicheze katika ligi baada ya kupata matatizo ya kifamilia yaliyomsababishia ashindwe kuungana na timu hiyo katika maandalizi ya mchezo.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems alisema kuwa beki huyo juzi Alhamisi jioni alijiunga na kambi ya timu hiyo na jana asubuhi alifanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo wa ligi.

Aussems alisema kuwa, mshambuliaji huyo amejiunga kwenye maandalizi ya timu hiyo baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia aliyoyapata na haraka akajiunga kikosini tayari kuwavaa wapinzani wao Ruvu.

“Mashabiki wa Yanga waondoe hofu juu ya Kagere, kwani tayari amejiunga kambini juzi Alhamisi na leo (jana) asubuhi alifanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ruvu.

“Hivyo, Kagere atakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachoivaa Ruvu katika kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri ya ushindi ambacho ndiyo kitu cha msingi kwetu,” alisema Aussems.

2 COMMENTS:

  1. Tafadhali ndugu muandishi pitia ulichokiandika kabla ya kuchapisha makosa ni mengi nimevumilia lakini sasa naona "is too much"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic