KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa yapo mengi ya kuzungumzia na sio kuhusu hatma ya kibarua chake ndani ya Simba.
Aussems aliondoka hivi karibuni kimyakimya jambo lilizozua maswali mengi juu ya hatma yake ndani ya Simba kutokana na timuatimua ambayo imepita kwa baadhi ya klabu.
Klabu ambazo zimewapiga chini makocha wao ni pamoja na KMC ambao wamemtimua Mwinyi Zahera, KMC Jakcson Mwayanja na Biashara United Amri Said.
"Najua kuna ambayo yametokea kwa baadhi ya timu hilo lipo wazi ila kwangu mimi siwezi kuzungumzia kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo yapo ya kuzungumzia.
"Nina kikosi kipana ambacho kina wachezaji wengi hilo ndilo ambalo ninalijua kuhusu hayo mengine siwezi kuzungumzia," amesema Aussems.
Aussems amerejea leo na kuanza kukinoa kikosi chake ambacho kitamenyana na Ruvu Shooting jumamosi uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment