REKODI ya
mabao 23 aliyoweka mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere imekuwa ikimpa taabu
kutokana na ugumu wa ligi ulivyo kwa sasa ndani ya ligi pamoja na kufikiria
namna ya kuipa mataji timu yake.
Kwa sasa
Kagere ambaye ni raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao nane timu yake ikiwa
imecheza jumla ya mechi 9 ikiwa na pointi 22 kibindoni.
“Ushindani
ni mkubwa kwa sasa kila mchezaji ana malengo yake kwangu mimi lengo la kwanza
ni kuipa mataji timu yangu kisha suala la ufungaji litafuata maana nikifikiria
tuzo itakuwa haina maana kwangu.
“Kwa sasa
tupo tayari kwa ajili ya ushindani na kufanya kazi kwa ajili ya kupata matokeo,
tunajua mashabiki wanahitaji nini nasi tunahitaji nini waendelee kutupa
sapoti,” amesema Kagere.
0 COMMENTS:
Post a Comment