JUMA
Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa licha ya kikosi chake kuwa na
mwendo wa kusuasua kitarejea kwenye ubora wake.
Mbeya City
imecheza jumla ya mechi 10 ina pointi 8 imeambulia ushindi mechi moja pekee na
kupata sare tano vichapo mechi nne ikiwa nafasi ya 18.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa ni suala la wakati kwa timu yake
kurejea kwenye ubora kwani kwa sasa anapitia kipindi cha mpito.
“Tunapitia
kipindi kigumu cha mpito kutokana na kutengeneza timu upya, wachezaji wana uwezo
na ninawaamini katika kupambana kupata matokeo.
“Kumekuwa na
shida kwenye safu ya ulinzi pamoja na ushambuliaji kwa kuwa matatizo
tumeyatambua tutatumia muda mwingi kujiaandaa kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata,”
amesema Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment