JURGEN Klopp, kocha mkuu wa Liverpool amesema kuwa hana mpango wa kufikiria rekodi badala yake anafikiria ushindi kwenye mechi zake anazocheza.
Liverpool ipo kileleni kwenye Ligi Kuu England ikiwa na pointi zake 37 baada ya kucheza mechi 13 imeshinda 12 na kutoa sare moja pekee ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Manchester United.
Klopp amesema:-"Siangalii kuhusu rekodi zinasema nini wala haziniumizi kichwa kwangu kitu muhimu ni kushinda na kupata matokeo chanya basi hayo mengine yatakuja yenyewe," amesema.
Jumatano Liverpool itashuka uwanjani kumenyana na Napoli mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wao wakiwa ni mabingwa watetezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment