November 26, 2019


Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameshindwa kujizuia na kujikuta akipagawa na kuweka hisia zake wazi juu ya wimbo wa staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

Lulu amejikuta akipagawa na Wimbo wa Mshumaa wa Kiba baada ya kuona vijana wake wa Kundi la Kings Music wakiuimba wimbo huo laivu kwa kutumia gitaa.

Lulu alitupia video fupi ya jamaa hao kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ikiwaonesha Cheed na Tommy Flavour wa Kings Music wakiimba wimbo huo kisha aliandika;

“Niko mahali kwenye ukuta wa chupingi, najikuna vipele vya baridi (goose bumps).”

Hata hivyo, Lulu aliungwa mkono na staa mwenzake wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu ambapo naye kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram alionekana akiongea na Kiba kupitia video call ya Mtandao wa WhatsApp kisha akaandika; “Na mniache, asante kwa hii track.”

Naye mwigizaji Esha Buheti aliandika; “Weee Ali (Kiba) sikuachii mpaka kufa.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic