NAY WA MITEGO AFURAHIA KUITWA FREEMASON
Mwanamuziki mwenye sauti ya mtetemo kunako Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema, watu wakimuita yeye ni mfuasi wa Freemason huwa anafurahi na kutamani kuwaambia wanaomuita hivyo, wakaribie kwenye ulimwengu huo.
Akistorisha na Gazeti la Ijumaa, Nay amesema, watu wengi wanamuita hivyo kwa sababu ya namba yake anayopenda kuitumia ya 996, lakini kwa upande wake anafurahi sana akiitwa hivyo kwa sababu wanamuita nao wanatamani ndiyo maana wamempachika jina hilo.
“Wakiniita Freemason, mimi nafurahi mno, tena sana kwa sababu hiyo ndiyo chata waliyonipa kwa sababu tu ya namba yangu ile ya 996 na nina imani wengi tu wanatamani kuingia huko,” alisema Nay anayekimbiza na Wimbo wa Mungu Anakuona.
0 COMMENTS:
Post a Comment