November 22, 2019



Ole Gunnar Solskjaer kocha mkuu wa Manchester United amesema kuwa hajashtuka kufutwa kazi kwa kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ambaye amefutwa kazi ndani ya kikosi hicho kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho.

Manchester United inaelezwa kuwa wameanza kuiwinda saini ya Pocchetino ili awe bosi wao mpya ndani ya kikosi cha Manchester United kilicho chini ya Solskjaer kwa sasa.

 “Kufukuzwa kwake ndani ya Tottenham hakujanishtua kwa sasa kwani alikuwa anafanya kazi zake nami pia nafanya kazi zangu kwa sasa nimefanya kazi kwa umakini na nimekuwa bora katika kile ninachokifanya.

“Haijalishi ni nini kimetokea kwake na nini ambacho mimi nakifanya bado nitaendelea kufanya vizuri na kupambana kwa ajili ya timu yangu, nimeona amepewa kazi Mourinho ninamtabua na uwezo wake ni mkubwa,” amesema.
Manchester United kwenye Ligi Kuu England ipo nafasi ya 7 ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 imejikusanyia jumla ya pointi 16 ikiachwa kwa pointi 18 na kinara wa ligi ambaye ni Liverpool.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic