November 17, 2019



TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kutupa kete yao ya pili kwenye mechi ya kufuzu Afcon Novemba 19 dhidi ya Libya mchezo utakaochezwa nchini Tunisia.

Rekodi zinaonyesha kuwa nyota ya Stars imeipoteza kwa mbali nyota ya Libya kwenye mechi zao za kimataifa hivyo endapo wachezaji watakaza zaidi ya walivyowafanyia Equatorial Guinea basi watashindwa wenyewe kuchagua idadi ya mabao ya kuwabugiza wapinzani wao.

Kwenye mechi nne za hivi karibuni ambazo Libya imecheza haijapata ushindi wa jumla zaidi ya kuambulia sare mechi mbili na kupoteza mechi.

Mechi yao dhidi ya Afrika Kusini Libya ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kabla ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Morocco pamoja na sare ya bila kufungana na Mauritania na ilipoteza mchezo wake wa juzi mbele ya Tunisia kwa kufungwa mabao 4-1.

Libya imefungwa mabao saba huku wao wakifunga jumla ya mabao matatu katika mechi zao nne wakipotezwa na Stars ambao kwenye mechi nne imeshinda moja na kulazimisha sare tatu na safu ya ushambuliaji ya Stars imefunga mabao manne na kufungwa mabao matatu pekee.

Matokeo ya Stars yapo namna hii:Tanzania 2-1 Equatorial Guinea, Rwanda 0-0 Tanzania
Tanzania 1-1 Burundi,Burundi 1-1 Tanzania kwenye kundi J ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu huku Libya ikiwa nafasi ya nne haina pointi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic