BONIFACE Mkwasa, kaimu Kocha wa Yanga amesema kuwa atatumia mchezo wa leo mbele ya Coastal Union kuendela kupanga kikosi chake cha ushindani ndani ya ligi.
Yanga leo Novemba 17 itashuka uwanja wa Uhuru kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Coastal Union majira ya saa 10:00 jioni.
Mkwasa amesema kuwa mechi za kirafiki zinawajenga wachezaji na kuwafanya wazidi kuimarika jambo ambalo anaamini litampa kikosi chenye maelewano.
"Tuna kazi kubwa ya kujenga kikosi na kila mchezaji ana uwezo jambo ambalo linanipa matumaini ya kuwa na kikosi bora chenye ushindani kwenye mechi zetu.
"Mechi za kirafiki ni nzuri kwa ajili ya kutengeneza muunganiko ningependa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi bado inaendelea," amesema.
Jumatano Yanga itakuwa kazini kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment