Imeelezwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Simba, Senzo Mazingisa, amesema kuwa klabu yao itakuwa na masharti ya kuhakikisha mchezaji wao analipwa na timu husika ambayo itapata nafasi ya kumsajili mchezaji wao dirisha dogo.
Dirisha hilo linatarajiwa kufunguliwa Disemba 15 na inatajwa kuwa baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi cha Simba wanaweza kwenda kwa mkopo kunako baadhi ya timu hapa Tanzania na nje ya nchi.
Taarifa zinasema kuwa Mazingisa ameeleza Simba haitoruhusu klabu itakayomsajili mchezaji wake kumlipa mshahara ambao ni tofauti na wanavyolipa wao, badala yake wamlipe sawa na ambao amekuwa akilipwa Simba.
Aidha, Mazingisa amesema Simba hawatahusika na kulipa mishahara tena ya wachezaji waliotoka kwa mkopo badala yake timu husika iliyomsajili itamlipa fedha hizo za mshahara.
Mmoja ya wachezaji wanaotakiwa ndani ya kikosi cha Simba kuelekea dirisha dogo ni Rashid Juma ambaye amekuwa akiwindwa na KMC iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment