KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana amesema kuwa
ilikuwa lazima wapate ushindi dhidi ya JKT Tanzania ili kuzidisha imani kwa
mashabiki wa klabu hiyo.
Yanga walipata ushindi wao wa nne msimu huu baada ya
kuwafunga JKT Tanzania kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa juzi, Ijumaa
kwenye uwanja wa Uhuru, Jijini Dar.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Patrick
Sibomana dakika ya
12, Juma Balinya dakika ya 23 na David Molinga aliyefunga
kwa faulo dakika ya 35, huku ya JKT yakifungwa na Adam Adam dakika ya 13 na
Danny Lyanga dakika ya 45.
Akizungumza na Spoti Xtra Sibomana alisema;
“Tangu tulivyoingia
uwanjani kila mchezaji alikuwa anajua lazima tushinde ili kujenga imani kwa
mashabiki, tunataka kuwaaminisha mashabiki wetu kuwa timu yao ni nzuri na wawe
na imani nayo.”
Yanga sasa wamecheza michezo sita na kuvuna alama 13,
wakishinda michezo sita, kupoteza mmoja na kutoka sare mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment