Uongozi wa klabu ya Yanga umeilalamikia bodi ya ligi kuwabadilishia ratiba ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania.
Awali ratiba ya mechi hiyo ilikuwa inapaswa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii lakini baadaye ikapanguliwa na kusogezwa nyuma ambayo ni leo Ijumaa.
Kufuatia mabadiliko hayo, Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema ni ratiba ambayo inaweza kuwaathiri kwa namna moja ama nyingine.
Mkwasa ameeleza ratina inapopangwa hata program zake za mazoezi huenda na muda hivyo panatokea mabadiliko kuna athari hutokea.
"Kiuhalisia ratiba inapobadilishwa kuna athari inaweza kutokea kwa namna moja ama nyingine.
"Ujue kila kitu kinakuwa kinapangwa kuendana na ratiba yenyewe, hivyo unapopanga kitu kisha unakuja kukipangua kuna namna vitu kadhaa haviwezi kwenda sawa."
Malalamiko yasiokwisha ndio urithi aliokuwachieni Zahera
ReplyDeleteyawezekana kweli iv hujui mnavipolo vingi mpaka ulalamike
ReplyDelete