November 27, 2019


Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Alliance Schools utakaopigwa jijini Mwanza Ijumaa ya wiki hii, mchezaji Mapinduzi Balama atakuwa nje ya dimba.

Balama atakuwa nje ya mchezo huo kufuatia kuumia nyonga katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya JKT Tanzania.

Taarifa zimesema kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amethibitisha kwamba Balama atakuwa nje ya kikosi sababu ya majeraha hayo.

Leo alfajiri kikosi cha Yanga kitaanza safari ya kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya aina yake kufuatia Alliance kuchapwa kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Azam FC jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic