December 4, 2019


AZAM FC itamenyana na Mtibwa Sugar visiwani Zanzibar kwenye sikukuu ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika Jumatatu ijayo, ikiwa ni mechi maalumu ya hisani ya kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu hizo mbili Ibrahim Rajab 'Jeba', aliyefariki dunia Septemba mwaka huu.

Mechi hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Bodi ya Ligi Zanzibar (ZFF) kwa kushirikiana na timu hizo zote mbili alizochezea Jeba, ambapo fedha zitakazopatikana kwenye mechi hiyo zitaenda kwa familia ya kiungo huyo.

Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Amaan, saa 2.00 usiku, Mtibwa Sugar watauza jezi namba 10 na 22 ambazo zilikuwa ni namba alizotumia Jeba wakati akiwa Mtibwa Sugar kwa kiasi cha shilingi 30,000 kwa jezi zenye jina na zisizo na jina kwa bei ya 20,000.


Pia Jeba amewahi kuzitumikia timu ya Taifa, Chuoni na Simba,

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic