LEO Uwanja wa Old Traford utawakutanisha wababe wawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Egland ambao kila mmoja kwa wakati wake alikuwa kwenye hali mbaya hivi karibuni.
Spurs ilikuwa na mwendo wa kusuasua lakini baada ya Mauricio Pochettino kupigwa chini kocha mpya Jose Mourinho ameanza kuirejesha kwenye mstari.
United wao mambo bado ni magumu kwani Ole Gunnar Solksjaer bado anaendeshwa na imani kwamba kesho atakuwa na kikosi imara.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa kuwa Mourinho alipigwa chini na United mwaka mmoja uliopita na leo anarejea uwanjani akiwa na timu nyingine ambayo ni Spurs.
Kwenye msimamo, Spurs ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 20 huku United ikiwa nafasi ya 9 zote zikiwa zimecheza mechi 14.
Mourinho amesema kuwa akishindwa kupata ushindi hawezi kuwa na furaha kwani hiyo ni asili yake hawezi kuibadili.
0 COMMENTS:
Post a Comment