December 4, 2019

MIRAJI Athuman ‘Sheva’ nyota wa Simba amesema kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.

 Sheva ambaye ukali wake umeanza kuonekana ndani ya Simba kwa msimu wake wa kwanza akitokea Lipuli, pacha yake na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere imehusika kwenye mabao 17 kwenye jumla ya mabao 19 ya timu hiyo msimu huu. Kagere amefunga nane na kutoa pasi mbili za mabao huku Sheva akifunga sita na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Sheva alisema kuwa kila mchezaji wa Simba ana ndoto za kutwaa ubingwa wa ligi jambo ambalo  linawafanya wapambane kufikia malengo yao.

“Ndoto za wachezaji wote wa Simba ni kuona kwamba tunatetea ubingwa ambao upo mikononi mwa Simba kwa sasa, haiwezi kuwa rahisi ndiyo maana tunapambana kupata matokeo chanya.

“Kikubwa ni kwa mashabiki kuendelea kutupa sapoti bila kuchoka nasi tutafanya kile ambacho wao wanapenda siyo kingine ni matokeo mazuri,” alisema Sheva.

Simba ipo kileleni ikiwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 10 za ligi, kwa sasa imefungwa jumla ya mabao matatu pekee, timu ya pili ni Kagera ambao wana pointi 24 wakiwa wamecheza michezo 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic