December 2, 2019

FRANK Domayo, nahodha msaidizi wa Azam FC, leo Desemba 2 amekwea pipa kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya tatizo la kuchanika msuli wa nyama ya paja.

Domayo alipata majeraha hayo, wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Azam FC imeeleza kuwa matibabu yake yatachukua muda wa siku 10 atakazokuwa huko, yakifanyika kwenye Hospitali ya Vincent Palotti chini ya Dr. Robert Nickolas.

Katika safari yake, Domayo ameambatana na daktari wa timu, Dkt. Mwanandi Mwankemwa.

1 COMMENTS:

  1. kila la heri Chumvi ukimtanguliza Mungu kwa kila hatua maana madaktari wanatibu lakini Mungu ndiye mponyaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic