December 2, 2019

LICHA ya Mrisho Ngasa kiungo mshambuliaji wa Yanga kupachika bao la kuongoza dakika ya 73 akimalizia pasi ya Patrick Sibomana limewazuia Yanga kusepa jumla na pointi tatu baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa taifa kukamilka kwa sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya KMC.

Ngasa aliingia kipindi cha pili dakika ya 45 akichukua nafasi ya Sadney Urkhob na alitumia dakika 28 kufunga bao la kuongoza lililozama kimiani.


KMC iliyo chini ya Mohamed Ally licha ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza na dakika ya 88 ilipata faulo iliyopigwa kiufundi na Hassan Kabunda haikuzaa matunda kwa kuwa iligonga mwamba na kurejea uwanjani.

Iliwabidi KMC watumie dakika 17 kurudisha bao hilo baada ya kupata penalti dakika ya 90+3 kutokana na mwamuzi kutafsiri kitendo cha beki kisiki Kelvin Yondani kumchezea rafu Kabunda ndani ya 18.

Bao pekee la KMC lilifungwa na Abdul Hilaly kwa mkwaju wa penalti na kuifanya KMC igawane pointi moja na Yanga.

Hii ni mara ya  kwanza kwa KMC kugawana pointi mbele ya Yanga kwani msimu uliopita ilifungwa nje ndani na kuacha pointi sita kwa Yanga kwenye mechi zilizochezwa uwanja wa Taifa.

2 COMMENTS:

  1. Viongozi wa Yanga ni wa kubeba lawama kwanini wanaruhusu wachezaji wao wa viungo waende Zanzibar Heroes halafu Azam wao hawakumruhusu kwenda mpaka walipocheza mechi yao na JKT....unajiuliza kwanini Yanga hawakupewa wachezaji wake lakini Azam walipewa wachezaji wao.....kuna aidha madhaifu ya Uongozi na uzembe wa kuwasiliana na Bodi ya Ligi kupata ratiba za ligi na marekebisho ya mechi. Bado Kocha Mpya anarudia makosa ya zamani kutobadilisha makosa ya defense midfield kufanya makosa yale yale na kusababisha mzigo kwenye mabeki wa kati na upande wa mabeki wa pembeni.....sijui mazoezini wanafundishwa nini? Hitaji la Kocha Mpya ni wakati wake muafaka!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga SC msipofanya maamuzi magumu katika dirisha hili la usajili, mnaweza kujikuta mnayumba sana msimu huu.
      Niliwahi kuandika ..kikosi cha Yanga SC kwa sasa si kikosi cha kuipa hofu timu yoyote ligi kuu kwamsimu wa 2019-20. Ni kikosi ambacho kinampa mpinzani chaguo la kwanza kusaka ushindi na chaguo la pili kujilinda endapo chaguo la kwanza likifeli.
      Kwa asilimia kubwa kikosi kimetawaliwa na averaged players ambao hawana madhara makubwa wakiwa na mpira wala wasipokuwa na mpira sema tu timing ikiwa nzuri na mpinzani akiyumba na jina anapigwa .
      Ligi ya msimu huu ni ngumu sana , takribani timu nne zinashuka daraja kubaki na timu 16 kwa msimu wa 2020-21 hivyo kila timu inacheza mechi zake kama fainali kujiweka sawa katika makusanya ya points.

      Yanga inahitaji kuwa na si chini ya wachezaji 6 bora na imara kuweza kuwabeba kuimaliza ligi salama na mashindano mengine.

      Walinzi wawili kushoto na kulia wenye sifa za wing back kwa wanaojua kusaidia timu kuwa na mashambulizi bora ya upande pia kuimarisha ulinzi kama jukumu la msingi.

      Eneo la kiungo; Yanga inahitajika kuwa na playmaker bora mwenye uwezo wa kusimamia mfumo wa kushambulia wa timu na pia kuinasua timu kwenye locks za wapinzani wao endapo mfumo wao wa kushambulia ukizibiwa njia . Mchezaji mahiri anayeweza kuiunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji pande zote .
      Yanga inahijika kuwa na washambuliaji wawili imara wenye uwezo wa kufunga katia ratio ya 2:1 . Wachezaji wenye kuipa pressure backline ya wapinzani wao .

      Wa mwisho ni mchezaji kiraka hususani eneo lao lote la kiungo cha chini , ulinzi wa kati na pembeni.
      Lazima kwa historia na ukubwa wa klabu hiyo iwe na kikosi cha ushindani . Kikosi ambacho mpinzani wako anajipanga kwanza kukuzuia kupata ushindi huku akivizia uoneshe makosa ajitutumue sio unakuwa na kikosi ambacho kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho mpinzani wako anacheza kwa kujiamini akisaka ushindi bila hofu.
      Fanyeni maamuzi magumu kwa masilahi mapana ya timu na klabu kwa ujumla . Kikosi kifanyiwe postmortem upya ili kuleta balance nzuri kimbinu na kiufundi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic