FT: Yanga 1-1 KMC
Ngassa dak ya 73 Goool kwa Yanga
Abdul Hilary dak ya 90+4 penalti
Goool linapachikwa na Abdul Hilary
Dakika ya 90+3 Kabunda anachezewa rafu baada ya kuchezewa rafu na Kelvin Yondan anapewa penalti
Dakika 90 zinakamilika zinaongezwa 4
Dakika ya 90 Sibomana anapasiha faulo
Dakika ya 88 Kaseke anachezewa rafu nje kidogo ya 18
Dakika ya 87 KMC wanapiga kona haizai matunda
Dakika ya 85 Kapera anapiga nje akiwa ndani ya 18 akimalizia pasi ya Kabunda
Dakika 84 Kapera anachezwa rafu nje kidogo ya 18 haizai matunda
Dakika 82 Kabunda anapiga faulo ya kukomoa inagonga mwamba na kurudi ndani
Dakika ya 81 James Msuva anachezewa rafu nje kidogo ya 18
Dakika ya 80 Kenny Ally anamtafuta Msuva ngoma inaanuliwa na Jaffary Mohamed, Molinga anamchezea rafu Fuko
Dakika ya 76 James Msuva anaingia anatoka Serge.
Dakika ya 73 Ngassa anafunga Goooool akimalizia pasi ya Sibomana.
Dakika ya 72 Serge wa KMC anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 71 Tshishimbi anapiga pasi ndefu inatoka nje, Sonso anatoka anaingia Mapinduzi Balama
Dakika ya 70 Kaseke anacheza faulo kwa mchezaji wa KMC inapigwa na Fuko
Dakika ya 69 Shikalo anaanzisha mashambulizi kuelekea KMC, Kaseke anapiga pasi inayoanuliwa na mabeki wa KMC
Dakika ya 68 Serge anapoteza mpira ndani ya 18
Dakika ya 67 Kapera anapiga shuti kali linapa juu lango
Dakika ya 66 Kabunda anamchezea faulo Shikalo mlinda mlango wa Yanga, Lamine anachezewa rafu na Kabunda inakuwa faulo kuelekea KMC
Dakika ya 64 Tshishimbi anapoteza mbele ya Kabunda
Dakika ya 63 Kapela anarejea uwanjani
Dakika ya 61 Kelvin Yonda anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 60 Kapela yupo chini anapewa hudua ya kwanza baada ya kugongana na Yondani, anabebwa nje kwa machela
Dakika ya 59 Ismail Gambo wa KMC anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 57 Kabunda anapiga shuti linagonga mwamba
Dakika ya 56 Ngassa anafanya jaribio linakwenda juu
Dakika ya 55 Shikalo anaokoa shuti la Serge
Dakika ya 54 KMC inapata faulo eneo la karibu na 18iliyochezwa na Lamine kwake Kabunda.
Dakika ya 52 Sibomana anacheza faulo inapigwa na Fuko
Dakika ya 51 KMC wanapiga kona nyingie haizai matunda
Dakika ya 50 Kapela anafanya shambulizi halizai matunda na wanapiga kona inaokolewa na Shikalo
Dakika ya 49 Abdul Hillay anaingia kuchukua nafasi ya Samatta ambaye ametolewa kwa machela, Tshishimbi anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 48 Samatta anachezewa rafu na Tshishimbi
Dakika ya 46 Sibomana anapiga kona ndefu inaokolewa na mabeki wa KMC
Dakika ya 45 Ngassa ndani Urknob nje
HT
Yanga 0-0 KMC
Dakika 45 za mwanzo zimekamilika zinaongezwa dakika 2
Dakia ya 45 Jaffar anarusha mpira kwake Kaseke anapeleka ndani Jonatha anaokoa hatari
Dakika ya 42 KMC inapiga faulo ambayo haizai matunda
Dakika ya 38 Sibomana anapiga shuti kali linagonga mwamba, Sadney anamalizia inaokolewa na Jonathan Nahimana
Dakika ya 37 Sibomana anachezewa faulo
Dakika ya 36 Samatta anapoteza pasi akiwa nje ya 18.
Dakika ya 35 KMC wanapeleka mashambulizi kwa Yanga kupitia kwa mgungila
Dakika ya 34 Kaseke anatengeneza pasi kwa Molinga anapiga nje ya lango inakuwa ni goal kick
Dakika ya 33 beki wa KMC anaanua majalo kuelekea Yanga.
Dakika ya 32 Molinga anapiga shuti kali akiwa ndani ya 18 linapaa angani
Dakika ya 30 Sibomana anapeleka mpira ndani ya 18 inakutana na kichwa cha Molinga inaokolewa a mabeki inakuwa kona inapigwa na Kaseke inakuwa kona nyingine inapaishwa na Yondani.
Dakika ya 29 Shambulizi la Keny Ally linazuiwa na mabeki
Dakika ya 27 Tshishimbi anachezewa faulo na wachezaji wa KMC inapigwa na Sibomana haizai matunda
Dakika ya 26 KMC wanaotea
Dakika ya 25 Kijili anasepa na kijiji
Dakika ya 24 Yondani kwenye umiliki wa mpira kwakwe Shikalo anayeamsha majalo kwenda kwa KMC
Dakika ya 23 KMC wanatibua mipango ya Yanga kulifuata lango lao
Dakika ya 22 Juma Abdul, Yondan, Tshishimbi kwakwe Juma Abdul wanalifuata lango la KMC sasa mabekiwa wa KMC wanatibua
Dakika ya 21 Kabunda anatoa mpira nje
Dakika ya 18 Lamine anachezewa faulo na mchezaji wa KMC
Dakika ya 17, KMC wanaliandama lango la Yanga wanachokosa kwa sasa ni utulivu na umakini wa kumalizia nafasi wanzozipata
Dakika ya 17 Ally akiwa ndani ya 18 anapaisha mpira juu
Dakika ya 16 Mgungila anajikunjua shuti lake linakwenda juu
Dakika ya 15 Jonathan anaokoa hatari langoni mwake
Dakika ya 12 Samatta anapokwa mpira na Papy
Dakika ya 11 Juma anamimina maji ndani ya KMC inaokolewa
Dakika ya 10 Sibomana anapiga kona inaokolewa na mabeki wa KMC
Dakika ya 09 Kenny anacheza rafu kwa mchezaji wa Yanga
Dakika ya 08 Kabunda anamtengenezea nafasi Keny Ally shuti lake halizai matunda
Dakika ya 07 Sibomana anapiga shuti kali linaokolewa na beki ndani ya 18
Dakika ya 05 Kaseke anapoteza mpira ndani ya 18
Dakika ya 02 Kabunda wa KMC anafanya jaribio ndani ya 18 linadakwa na mlinda mlango
Yanga SC msipofanya maamuzi magumu katika dirisha hili la usajili, mnaweza kujikuta mnayumba sana msimu huu.
ReplyDeleteNiliwahi kuandika ..kikosi cha Yanga SC kwa sasa si kikosi cha kuipa hofu timu yoyote ligi kuu kwamsimu wa 2019-20. Ni kikosi ambacho kinampa mpinzani chaguo la kwanza kusaka ushindi na chaguo la pili kujilinda endapo chaguo la kwanza likifeli.
Kwa asilimia kubwa kikosi kimetawaliwa na averaged players ambao hawana madhara makubwa wakiwa na mpira wala wasipokuwa na mpira sema tu timing ikiwa nzuri na mpinzani akiyumba na jina anapigwa .
Ligi ya msimu huu ni ngumu sana , takribani timu nne zinashuka daraja kubaki na timu 16 kwa msimu wa 2020-21 hivyo kila timu inacheza mechi zake kama fainali kujiweka sawa katika makusanya ya points.
Yanga inahitaji kuwa na si chini ya wachezaji 6 bora na imara kuweza kuwabeba kuimaliza ligi salama na mashindano mengine.
Walinzi wawili kushoto na kulia wenye sifa za wing back kwa wanaojua kusaidia timu kuwa na mashambulizi bora ya upande pia kuimarisha ulinzi kama jukumu la msingi.
Eneo la kiungo; Yanga inahitajika kuwa na playmaker bora mwenye uwezo wa kusimamia mfumo wa kushambulia wa timu na pia kuinasua timu kwenye locks za wapinzani wao endapo mfumo wao wa kushambulia ukizibiwa njia . Mchezaji mahiri anayeweza kuiunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji pande zote .
Yanga inahijika kuwa na washambuliaji wawili imara wenye uwezo wa kufunga katia ratio ya 2:1 . Wachezaji wenye kuipa pressure backline ya wapinzani wao .
Wa mwisho ni mchezaji kiraka hususani eneo lao lote la kiungo cha chini , ulinzi wa kati na pembeni.
Lazima kwa historia na ukubwa wa klabu hiyo iwe na kikosi cha ushindani . Kikosi ambacho mpinzani wako anajipanga kwanza kukuzuia kupata ushindi huku akivizia uoneshe makosa ajitutumue sio unakuwa na kikosi ambacho kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho mpinzani wako anacheza kwa kujiamini akisaka ushindi bila hofu.
Fanyeni maamuzi magumu kwa masilahi mapana ya timu na klabu kwa ujumla . Kikosi kifanyiwe postmortem upya ili kuleta balance nzuri kimbinu na kiufundi.
Yanga katika hesabu take no kuwa ishinde michezo Yake yote na bila ya suluhu ndio wamgaragaze mnyama wanyakuwe ubingwa na huku Mnyama, Azam, Kagera na wengineo vinywa wazi
ReplyDelete