December 24, 2019


Licha ya awali kuelezwa kuwa mabosi wa Yanga wanapamba kunasa saini ya mchezaji, mshambuliaji kutoka UD do Songo, Luis Muquissone, inaelezwa Simba wako katika hatua za mwisho kumalizana naye.

Mchezaji huyo ambaye aliwafunga Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika raundi ya mchezo wa pili, amekuwa katika vichwa vya habari vingi nchini juu ya timu za Simba na Yanga.

Taarifa zinasema kuwa vigogo kadhaa wa Simba walishasafiri kuelekea Msumbiji kuweka mikakati kadhaa kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Licha ya wanayanga wengi kuamini kuwa mchezaji huyo anaweza kutua kwao, hali inazidi kuwa tofauti kutokana na kuendelea kubadilisha upepo na inaonesha zaidi ya asilimia 95 anaweza kutua Simba.

4 COMMENTS:

  1. Kidomodomo chao ndicho kilichowaponza Yanga.Tulisema Yanga hawana umbavu wa kugombania mchezaji na Simba kama kweli Simba watamuhitaji mchezaji husika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa uwekezaji mkubwa wa MO pale Simba huyu mchezaji, japo sio mbaya, lakini sio wa kiwango cha kusema wa kutunishiana misuli na Yanga. Nauona kama usajili wa kishabiki zaidi kuliko kuangalia mahitaji ya timu.

      Simba inahitaji pure goal getter na ndio maana utaona Bocco alivyokuwa na majeraha Simba ilipwaya sana kiufungaji. Kina Chama, Kanda, Shiboub ni wachezaji wazuri ni wa kiwango kilekile cha Niyonzima ambaye alitemwa kimakosa sana.

      Ilikuwa ni heri zaidi kumbakisha kundini Niyonzima kwa gharama nafuu kuliko kumleta mchezaji wa kiwango kilekile kwa gharama za juu. Na ndio maana naona Yanga waliliona mapema na kuamua kuachana naye!

      Delete
    2. Umenena kweli.Yule mchezaji ni wa kiwango cha kawaida mno hana uwezo wa kutisha kuliko hata wachezaji wazawa waliopo.Inawezekana ni habari za blog hii kujaza habari kwenye taarifa zao lakini si kweli kama Simba wanamhitaji

      Delete
  2. Niliwabi kusikia kuwa huyo mchezaji alidokezwa na wasioitakia wema Wana Jangwani utata sugu uliokuepo huko wa kutokulipwa wachezaji na makocha haki zao ikabidi we ngi kuondoka au kuondoshwa Bila ya stahiki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic