December 24, 2019


Uwepo wa Ghalib Mohammed katika kampuni ya GSM ndani ya Yanga unaonekana kudhamiria kuiboresha timu hiyo kwa kasi ambapo inaelezwa hivi sasa wanapambana kuwania saini ya winga wa TP Mazembe.

Tetesi zinasema kuwa mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara zinasema kuwa Yanga wameanza kuwania saini ya winga Gnanzou Djeni.

Winga huyo kutoka taifa la Ivory Coast ameanza kuvutiwa waya na Yanga ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwa muda mrefu ndani ya kikosi hicho.

Kukosa namba kwa mchezaji huyo kumemfanya awe katika mikakati ya kutaka kuhama ili aelekee mahala pengine kwa ajili ya kulinda kipaji chake.

Sababu hizo zinawafanya Yanga wazidi kutia nguvu ili kupata saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kuja kuboresha kikosi cha Yanga ambacho kimekuwa kikifanya usajili wa wachezaji wapya.

4 COMMENTS:

  1. Kama Yanga wanataka kusajiri ambaye huwa hapati nafasi ya kucheza , basi waje wanisajiri na mimi huwa sipati nafasi ya kucheza mtaani kwetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hupati nafasi ya kucheza vigodoro stejini au?

      Delete
  2. Kweli Wana yanga wana ubavu wa kuwapiku mamilionea wa Mazembe na kuchota nyota wao

    ReplyDelete
  3. Inaminiika kelele za Yanga za kila siku za kusajili babu kubwa ni kuamini kwao kuwa itaweza kumteka Mnyama kisaikolojiya wakati wachezaji Hoi hawajalipwa stahaki zao Hahahaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic