Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kwamba hakuna laini ya simu itakayofungwa kabla ya tarehe hiyo. Aidha, imesema wananchi wanatakiwa kwenda kusajili laini zao kwa kutumia vitambulisho vya uraia, na kuthibitisha usajili huo kabla ya muda uliowekwa kwa kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kuzifunga.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakanjala, alisema hadi sasa laini za simu milioni 20 zimesajiliwa; “Hakuna mabadiliko yaliyotolewa ikifika Disemba 31, 2019, laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) na kuthibitisha kwenye mifumo zitafungwa, tunawakata wananchi wasajili haraka,” alisema.
Aidha, alisema hakuna mtoa huduma atakayeruhusiwa kufunga au kukatisha mawasiliano ya mtumiaji yeyote kabla ya muda uliopangwa.
Jana kwenye baadhi ya makundi songezi (WhatsApp) baadhi ya watumiaji wa laini za simu walilalamika kukosa mawasiliano kwenye baadhi ya laini kwa kile kilichoelezwa kuwa zimezimwa kwa kuwa hawajasajili.
Mei mwaka huu, serikali ilitangaza ulazima wa usajili wa laini za simu, na kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu zitafungwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment