December 21, 2019


Mambo ni moto ndani ya kikosi cha Simba. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kwani muda wa maisha ya beki wa kati wa timu hiyo raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa wa kuendelea kuwa katika kikosi hicho kuanza sasa umeanza kuhesabika.

Wawa ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita inadaiwa kuwa msimu huu ndiyo msimu wake wa mwisho katika kikosi hicho, hivyo uongozi wa timu hiyo tayari umeanza harakati za kusajili mbadala wake haraka iwezekanavyo.

Habari ambazo Championi Ijumaa limezipata zimedai kuwa, uongozi tayari upo katika hatua za mwishomwisho za kumalizana na beki wa kati wa Coastal Union ya Tanga, Bakari Mwamnyeto ambaye pia Yanga inadawa kumwania ili kuja kuchukua nafasi hiyo ya Wawa.

“Uongozi umefika hatua hiyo baada ya kuanza kuona uwezo wa Wawa unapungua kutokana na umri alionao ambao sasa unamfanya kiwango chake kishuke.

“Kwa hiyo Mwamnyeto ndiye anayekuja kuchukua nafasi yake, lakini anatarajia kuja mapema katika dirisha hili dogo la usajili ili aweze kuzoea mapema utamaduni wa soka la Simba ili mpaka kufikia msimu unaokuja awe tayari ameshazoeana na wenzake, hata Wawa akiondoka pengo lake lisionekane,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ili aweze kuzungumzia hilo hakupatikana, kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic