December 4, 2019


VIRGIL Van Dijk beki wa Liverpool amesema kuwa hajawahi hakuwahi kufikiria kama siku moja kama anaweza kuwa kwenye orodha ya wachezaji bora duniani wanaowania tuzo kubwa ya Ballon d'Or.

Dijk ameshika nafasi ya pili kwa ubora huku namba moja ikiwa kwa Lionel Messi raia wa Argentina anayekipiga Barcelona na nafasi ya tatu ipo kwa Cristiano Ronaldo.

Dijk amesema: "Sikufikira na wala sikudhani kwamba siku moja nitakuwa hapa mpaka pale nilipotajwa, nimefurahi na nitazidi kupambana kwa ajili ya kuwa bora zaidi.

"Mafanikio yetu ndani ya timu ya Liverpool mwaka jana na timu ya taifa ya Uholanzi, nina amini mwakani nitafanya vema zaidi.

"Kwa upande wa Messi ni mchezaji bora kwani ameweza kunipita hata mimi, kutwaa tuzo sita si mchezo ni kitu cha heshima," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic