December 28, 2019


Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema kiu yake nikuona kikosi hicho kinapata ushindi wa mabao mengi zaidi ya waliyopata kwenye mechi iliyopita waliyoshinda 4-0 dhidi ya Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Simba ilitawala mchezo kwa asilimia kubwa hasa katika kipindi cha pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha huyo aliyeiongoza Simba kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu alisema: “Wachezaji wangu wamecheza na kuonesha kiwango kikubwa cha kumiliki mpira, lakini sijaridhishwa na ushindi tuliopata kwakuwa kiu yangu nikuona tunapata ushindi wa pointi tatu kwa mabao mengi, malengo yetu nikuona kila sehemu inatimiza majukumu yake kuwapa mashabiki furaha,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Alisema kipindi cha pili wakati wanaingia alifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji wawili kwa mpigo, Jonas Mkude na Francis Kahata na kuwaingiza Mzamiru Yasini na Deo Kanda na walibadilisha mchezo na kuifanya timu kuwa na kasi na kufunga mabao matatu ndani ya dakika chache.

Alisema bado anakazi kubwa ya kuboresha sehemu mbalimbali hususan kwenye ushambuliaji ili kuhakikisha nafasi nyingi zinazotengezwa ziwe zinatumiwa ipasavyo.

3 COMMENTS:

  1. iandae timu vizuri kocha wetu tunakuamini than safu ya ulinzi ikiongozwa na wawa imekuwa putu sana so tukikutana na timu yenye kiu ya kufunga kama kmc tutapa shida kidogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio kmc mbona unazunguka?? weka bayana kua tukikutana na yanga tutapigwa kama watoto

      Delete
  2. Yanga jiandaeni kisaikolojia,ikiwezekana hiyo siku kimbieni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic